Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Omari Kipanga Septemba 26, 2024 ametembelea Chuo cha VETA cha Mkoa wa Mara na kukutana na menejimenti ya Chuo hicho kuzungumzia kazi utoaji Elimu Chuoni hapo.
Naibu Waziri huyu amekagua karakana na madarasa kujionea ujifunzaji kwa vitendo ikiwa ni utekekezaji ahadi aliyoitoa bungeni kwa mbunge wa jimbo musoma mjini Bw. Vedastus Manyinyi kutembelea Chuo hicho kuona hali ya chuo na hali ya ufundishaji na ujifunzaji pamoja na changamoto zilizopo.
Aidha ameahidi Wizara itazifanyia kazi changamoto hizo ili kuhakikisha mafunzo ya ujuzi yanayotolewa katika Chuo hicho yanaendelea kuwa bora pamoja na kuongeza miundombinu ikiwemo karakana na zana za kufundishia