Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Nchini Dkt. Thomas LeBlanc ambapo wamejadiliana juu ya masuala mbalimbali ya elimu.



Majadiliano hayo yamefanyika Januari 08, 2025 jijini Dodoma, ambapo viongozi hao wamezungumzia vipaumbele mbalimbali katika kutekeleza mageuzi ya elimu baada ya USAID kuchukua jukumu jipya la kuwa Mwenyekiti wa Kikundi cha Washirika wa Maendeleo ya Elimu kuanzia Januari, 2025, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) ikihudumu kama Mwenyekiti mwenza