Zaidi ya Shilingi bilioni 4 zimetumika kufanikisha ujenzi wa majengo mapya 11 katika Chuo cha Ualimu Dakawa.



Akizungumza Aprili 26, 2026 mjini Morogoro wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amesema kuwa ujenzi huo unafanyika kwa awamu, ambapo mpango ni kujenga jumla ya majengo 32.



Prof. Mushi ametaja majengo hayo kuwa ni Jengo la Utawala lenye ofisi na ukumbi wa mkutano, madarasa nane yenye uwezo wa kuchukua walimu tarajali 360, bweni jipya lenye uwezo wa kuchukua walimu tarajali 250, pamoja na bwalo la chakula lenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 1000 kwa wakati mmoja. Aidha, ujenzi wake umefikia asilimia 92.