
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, akishirikiana na Naibu Katibu Mkuu Prof. Daniel Mushi pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu, wamefanya ukaguzi ili kujiridhisha na utayari wa shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Chuo cha Ualimu Dakawa.

Tukio la uwekaji wa jiwe la msingi linafanyika leo, Aprili 26, 2026, likiongozwa na Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Hafla hiyo inatarajiwa kuwa hatua muhimu katika kuimarisha miundombinu ya elimu na kukuza ubora wa mafunzo ya ualimu nchini.


