
Mwenyekiti wa Jopo la Majaji Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, 2025/2026 amesema kuwa mchakato wa tathmini na uhakiki wa miswada ulifanyika kwa uwazi, haki na weledi.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa Tuzo hizo Aprili 13, 2026 Jijini Dar es Salaam amesema kuwa zoezi hilo lilichukua takribani miezi mitatu, kuanzia Januari hadi Machi 2023, ambapo walianza kwa kwa kuweka vigezo vya msingi vya kutathmini kazi za fasihi.

Amefafanua kuwa Vigezo hivyo vilijumuisha vipengele maalum na alama za msingi, huku kamati ikitoa misimbo ya usiri ili kuhakikisha majaji wanatathmini miswada kwa usawa na bila ushawishi wa nje.
Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa jumla ya majaji 12 walihusika katika mchakato huo, wakiwa wamegawanywa katika makundi matatu kwa kila fani: ushairi, tamthiliya, riwaya na fasihi ya watoto. Kila jaji alichunguza miswada yote katika fani yake na kuweka alama kwa kutumia vigezo vilivyowekwa.

Mwenyekiti amehitimisha kwa kueleza kuwa kazi ya majaji ilifanywa kwa umakini mkubwa, ikijumuisha mijadala mikali na mashindano ya hoja kabla ya kufikia uamuzi wa mwisho.
Amesisitiza kuwa lengo kuu lilikuwa kuhakikisha washindi wanapatikana kwa haki na kwa kuzingatia viwango vya fasihi na elimu, na kwamba mchakato mzima ulilenga kuimarisha uandishi bunifu na kuendeleza fasihi ya Kiswahili kwa vizazi vijavyo

