
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda ameongoza kikao cha Wadau wa Elimu ya Ufundi na Ufundi Stadi, Elimu ya Juu pamoja na Taasisi Rekebu kujadili mwelekeo wa utekelezaji Mkakati wa Ushirikiano kati vyuo na ulimwengu wa kazi.

Kikao hicho kimefanyika Machi 10, 2026 jijini Dodoma, na kuhudhuriwa na Naibu Waziri Mhe. Wanu Hafidh Ameir na viongozi mbalimbali kutoka Taasisi.

Katika kikao hicho wataalamu kutoka Benki Kuu ya Tanzania pia waliwasilisha andiko kuhusu programu ya kuwezesha Vijana wahitimu wa Mafunzo ya Ufundi na Ufundi Stadi kupata mikopo kuendeleza Biashara wanazoanzisha baada ya kuhitimu.

Programu hiyo pia inahusisha kuanzisha Kongani za ujuzi zitakazo wezesha vijana kupata fedha na kuanzisha biashara, na/au kuendeleza bunifu zilizopo na kuzibiasharisha.


