Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH na Benki ya CRDB imetenga jumla ya Shilingi bilioni 4.6 kuwapatia mitaji vijana wabunifu kupitia Mfuko wa Samia wa Ubiasharishaji Ubunifu ulioanzishwa mwaka 2024. Mfuko huo umetambua wabunifu 3,300 nchini, huku 300 wakiendelezwa kupitia MTUSATE, ukilenga bunifu zilizo tayari kuingia sokoni lakini zinakosa mtaji.



Akizungumza Dar es Salaam, Naibu Waziri Wanu Hafidhi Ameir amesema mfuko unalenga kuongeza ushindani wa wabunifu sokoni na kuchochea ajira pamoja na ukuaji wa uchumi. Hata hivyo, katika kipindi cha miezi 10, vijana saba pekee wamefanikiwa kupata mikopo huku kiasi kidogo tu cha fedha kilichotengwa ndicho kimetumika, hali inayoonyesha mwitikio bado ni mdogo.



Ambapo baadhi ya wanufaika ni pamoja na Paul Kitema na George Buchafwe, huku Serikali ikiendelea kutoa wito kwa vijana wengi zaidi kuwasilisha maombi ili kunufaika na mitaji hiyo, kubadili bunifu kuwa biashara endelevu na kuongeza mchango wao katika uchumi wa taifa