Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera amekutana na kufanya mazungumzo na Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Elimu za Mawali, Zambia na Zimbabwe waliopo Nchini katika ziara ya kujifunza.
Wizara hizo zinalenga kujifunza namna Sera ya Elimu inavyotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na wadau kipekee ushirikiano na shirika la CAMFED katika kuwarejesha shuleni wasichana waliokatishwa masomo.
Kikao hicho kimefanyika septemba 23, 2024 Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu katibu Mkuu kutoka OR TAMISEMI Bw. Atupele Mwambene na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa