Mkurugenzi wa Elimu Maalum Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Magreth Matonya amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023 imezingatia stahiki mbalimbali kwa wenye mahitaji Maalum kuhakikisha wanapata elimu bora kuchochea maendeleo yao.



Dkt. Matonya ameeleza hayo leo Septemba 20, 2024 jijini Arusha akitoa taarifa kuhusu Maadhimisho ya Miaka 30 ya Elimu Jumuishi, ambapo amesema yamelenga kutangaza mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.



Dkt. Matonya ameongeza kuwa, Maadhimisho hayo yamewapatia nafasi watafiti na watalam kushiriki katika mijadala mbalimbali ili kuwezesha utekelezaji wa Elimu Jumuishi