Serikali, wadau na watalaam wa sekta ya elimu wamekutana Septemba 19,2024 jijini Dar es Salaam na kujadili vipaumbele katika kuboresha Sekta ya Elimu



Kati ya aeneo yaliyotajwa kuwa ya kipaumbele katika mjadala huo ni uendelezaji wa taaluma ya ualimu na ajira, mazingira ya utoaji elimu na uwajibikaji.



Kwa upande wa Taaluma ya Ualimu imeelezwa kuwa Serikali imeanza utekekezaji wa Mradi wa GPE (TSP) wenye thamani ya Dola 167 milioni (zaidi ya Sh454.04 bilioni), unafadhiliwa na Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE).



Hayo yameelezwa leo, Septemba 19, 2024 na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) katika kikao hicho amabacho pia kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Charles Mahera



Kwa upande wake Meneja Programu Mwandamizi wa GPE kutoka Ubalozi wa Sweden, Stella Mayenje amesema hii ni mara ya pili Tanzania kunufaika Mradi huo ambapo awali ilipata Dola 84 milioni (zaidi ya Sh228.3 bilioni)