Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Septemba 11, 2024 ametembelea Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kasulu na kukagua karakana zinazotumika kutoa mafunzo kwa vitendo katika fani mbalimbali zinazofundishwa katika Chuo hicho.



Katika ziara hiyo Prof. Nombo ameambatana na wawakilishi kutoka Ubalozi wa Canada Nchini Tanzania (Global Affairs Canada) Bi. Stephanie Brunet na Bi. Rasmata Barry.



Viongozi hao wapo Mkoani Kigoma Wilayani Kasulu kwa ajili ya Kikao cha Kamati tendaji (Program Steering Committee) ya Mradi wa Uwezeshaji Kupitia Ujuzi (ESP) unaotekelezwa katika baadhi ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) Nchini.

-