Baadhi ya Wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari wanashiriki katika mkutano wa wadau wa kutoa maoni katika rasimu ya mapitio ya Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu 2021/2022 - 2025/2026 unaoendelea Agosti 20, 2024 Jijini Dar es Salaam.
Katika Mkutano huo Wanafunzi kutoka Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Kati, Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Elimu ya Juu wamepewa nafasi ya kujadili na kutoa maoni ya nini wanataka kukiona katika mpango huo kwa lengo la kuboresha mchakato mzima wa ufundishaji na ujifunzaji ili kuwa na wahitimu wenye ujuzi na umahiri.