Viongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Taasisi zilizo chini ya Wizara, Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu vya Umma pamoja na Watumishi Agosti 09, 2024 walipata fursa ya kumuaga rasmi aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe aliyestaafu.
Halfa ya kumpongeza na kumuaga Prof. Mdoe ilifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dodoma ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda, Naibu Waziri Mhe. Omari Kipanga, Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula walielezea namna walivyofanya naye kazi kwa ushirikiano na kumtakia maisha mema na mafanikio.
Prof. James Mdoe alishukuru kwa ushirikiano aliokuwa akiupata wakati wa utumishi wake katika Wizara ambayo alihudumu kwa kipindi cha takriban miaka nane na kwamba mafanikio ambayo aliyapata yalitokana na ushirikiano alioupata kutoka kwa kila mtumishi katika Wizara hiyo.