Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Agosti 04, 2024 amewasili katika eneo la Maekani Kampasi Kuu Morogoro kushuhudia uwekaji wa Jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Chuo Kikuu Mzumbe utakaofanywa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.