Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Franklin Rwezimula wamewasili mkoani Rukwa kwa ajili ya kushiriki ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Viongozi hao leo Julai 14, 2024 wamekagua Chuo cha Ualimu Sumbawanga, Chuo cha Ufundi VETA cha Mkoa wa Rukwa pamoja na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Kampasi ya Rukwa (MRCC) ambapo Rais anatarajiwa kutembelea Taasisi hizo.



Aidha, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Chuo cha Ualimu Sumbawanga na kuweka jiwe la msingi katika Chuo cha Ufundi VETA cha Mkoa wa Rukwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Kampasi ya Rukwa.