Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amesema matokeo ya ubunifu wa Teknolojia mbalimbali zilizojipambanua katika Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ni kielelezo tosha cha uwekezaji wa miundombinu ya kielimu ambayo imewekezwa na serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mhe. Batilda amesema hayo Mei 30, 2024 wakati akitoa salamu za mkoa huo ambapo amesema uwekezaji uliiofanywa katika sekta ya elimu umeleta matokeo chanya katika Mkoa huo.
Aidha ameongeza kuwa Mkoa huo utatekeleza mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na wadau wa Elimu ili kuongeza ufaulu katika Mkoa huo.