Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Elimu, Michezo na Utamaduni Mhe. Husna Sekiboko amesema Bunge la Tanzania linatamani kuona bunifu zinazoibuliwa zinaboreshwa ili zilete tija na kutatua chamamoto mbalimbali za kijamii.
Mhe. Sekiboko amesema hayo Mei 27, 2024 jijini Tanga wakati akizungumza katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu ambapo amesema kuwa mhimili huo unataka kuona Bunifu zinazoibuliwa hazibaki kwenye Maonesho pekee bali ziendelezwe na kufikia hatua ya kubiasharishwa ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kutoa hamasa kwa Wabunifu mbalimbali.
Amesema kuwa Maonesho ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yameibua fursa mbalimbali kwa Wananchi wa mkoa Tanga na Wadau wa maendeleo ambao wamejifunza teknolojia mbalimbali za kisasa katika kutekeleza majukumu yao.