Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Aprili 12, 2024 amempokea Mshindi wa Tuzo ya Nobel katika Fasihi Mwaka 2021 Prof. Abdurazack Gurnah ambaye anatarajiwa Mgeni Rasmi katika halfa ya utoaji Tuzo ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu 2024



Prof. Gurnah amesema amefurahi kuwa sehemu ya tukio hilo kubwa muhimu katika uhamasishaji wa uandishi na usomaji wa vitabu nchini.



Tuzo hizo ziliasisiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Mwaka 2023 na kuendeshwa na Taasisi ya Elimu Tanzania kwa lengo la kuhamasisha uandishi bunifu na usomaji vitabu, kutunza historia na utamaduni wa Mtanzania na kuinua sekta ya uchapishaji nchini.



Hafla ya utoaji tuzo hizo itafanyika Aprili 13, 2024 jijini Dar es Salaam ambapo Tuzo zitatolewa kwa Waandishi Bunifu wa Mashairi, Riwaya na Hadithi za watoto