Leo Januari 18, 2024 Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Misaada la Watu wa Marekani (USAID), Bw. Craig Hart.



Kikao hicho kimelenga kujadili ushirikiano katika kuimarisha sekta ya Elimu , utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo na Mitaala Mipya pamoja na kushirikiana katika kufanya mapitio ya programu na miradi wanazotekeleza.



katika kikao hicho
Waziri Prof. Mkenda ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Sayansi Prof. James Mdoe, Naibu Katibu Mkuu Elimu Dkt. Franklin Rwezimula, Mkurugenzi wa Mipango Atupele Mwambene , Kaimu Kamishna wa Elimu na Mkurugenzi wa Elimu Msingi Abdul Maulid ,Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Sylvia Lupembe na viongozi wengine