Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendelea kuimarisha ushirikiano na mashirika ya kimataifa na sekta binafsi katika kuboresha sekta ya elimu nchini.



Leo Januari 18, 2024 Jijini Dodoma Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu wa Wizara amefanya mkutano na Bw. James Mclntyre Mkuu wa masuala ya Elimu katika Shirika la Mastercard Foundation ambae pia aliambatana na Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda kutoka Shirika la Educate Bwana Kamanda kamiri.

Lengo kuu la mkutano huo lilikuwa ni kutambilisha taasisi hizo kazi wanazofanya na kubainisha maeneo mbalimbali ya ushirkiano katika Elimu, Sayansi na Teknolojia.