Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Caloryne Nombo akifafanua jambo katika kikao na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Mwenyekiti wake, Mhe Naghenjwa Kaboyoka jijini Dodoma.
Kamati hiyo imepitia na kuchambua taarifa ya ukaguzi wa kiufundi kuhusu ujenzi wa Shule za Sekondari kupitia mradi wa kuboresha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) unaotekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais TAMISEMI kikao hicho pia kimehudhuriwa na Katibu Mkuu OR- TAMISEMI anaeshughulikia Miundo Mbinu Mhandisi Rogatus Mativila.