Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla Leo Disemba 19, 2023 amefungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Skauti Tanzania uliofanyika Zanzibar Chini ya uenyekiti wa rais wa chama hicho Prof Adolf Mkenda ambae ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo amewataka wajumbe wa mkutano huo kutoa michango na uzoefu wao ili kuweka na mikakati imara ambayo itasaidia kuimarisha uskauti Tanzania.
Aidha, Makamu huyo wa Rais amewataka kuzingatia dhamana waliyonayo kikatiba katika kufanya maamuzi kupitia Baraza Kuu na kuzingatia hadhi na kanuni za Skauti bila kuweka maslahi binafsi.