Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa Dar es Salaam imetoa Tuzo Maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kutambua mchango wake katika kuleta mageuzi katika sekta ya elimu kwa kuelekeza kufanyika kwa Mapitio ya Sera na Mitaala ili iweze kulenga kutoa ujuzi.
Tuzo hiyo imepokelewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda kwa niaba ya Mhe. Rais.