Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Atupele Mwambene amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo 2023 pamoja na kulenga kujibu mipango na vipaumbele vya nchi yetu, imezingatia kuwajengea wahitimu ujuzi na umahiri ili kuwawezesha kushindana katika soko la ajira kitaifa na Kimataifa.

Mwambene ametoa kauli hiyo leo Novemba 27, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Uhuru FM kuhusu Sera mpya ya elimu