Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametembelea karakana mbalimbali katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji zinazotumika kufundishia na kujifunzia kwa vitendo



Prof Mkenda yuko katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kuzindua mpango wa Ufadhili kwa Wanafunzi wa Kike wanaosoma programu za Uhandisi katika Sekta ya Usafirishaji pamoja na kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa majengo matano ya chuo hicho yanayofadhiliwa na Mradi wa EASTRIP.