Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Oktoba 28, 2023 atazindua ufadhili (Scholarship) kwa Wanafunzi wa Kike wanaosoma programu za Uhandisi katika sekta ya usafirishaji pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo matano ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji yanayofadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano wa Kikanda wa Afrika Mashariki (EASTRIP).

Mradi wa EASTRIP unasimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni wa kikanda na umeshirikisha nchi tatu ambazo ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kenya na Ethiopia.

Lengo kuu la mradi wa huu ni kuongeza UBORA na UPATIKANAJI wa programu zinazotolewa katika Vyuo vya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi vya Kikanda (Technical and Vocational Education and Training -TVET) kwa kuanzisha Vituo vya Umahiri.