Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Serikali inaendelea kutekeleza kwa ufanisi mkubwa mipango na Miradi ya Elimu kupitia Vyuo vya Ufundi Stadi ili kuhakikisha Taifa linapata Vijana mahiri na wenye Ujuzi watakaoweza kulikabili soko la Ajira ndani na nje ya nchi.
Prof. Nombo ameyaeleza hayo mapema leo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu masuala mbalimbali ya kimkakati ikiwemo Mafunzo ya amali yanayolenga kuwaimarisha vijana na Ujuzi