Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda tayari awasili Viwanja vya Satellite City Nkokoto A, Killipo Chuo cha Ufundi Stadi Veta Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa ajili ya kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya uwekaji jiwe la Msingi la Ujenzi wa Chuo hicho.



Kuelekea shughuli hiyo muhimu inayotarajiwa kufanyika hapo kesho Prof. Mkenda aungana na Viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe. Sauda Mtondoo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Mhe. Husna Sekiboko pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaendelea na Ziara yake katika mikoa ya kanda ya Kati na Magharibi nchini, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la Ujenzi wa Chuo hicho.

Kwa taarifa juu ya tukio hili na mengineyo endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii.