Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo wamekutana na Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Nelson Mandela ya Sayansi na Teknolojia Omari Issa na Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Maulilio Kipanyula kujadili masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Chuo hicho.

Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma tarehe 12.09.2023 ambapo pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuhakikisha Chuo hicho kinaendelea kuwa bora na kuvutia Wanafunzi wengi kutoka ndani na nje ya nchi.