Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amewashukuru wadau wa elimu ambao kwa uzalendo wao wamechangia kwa dhati jitihada za Serikali kwa kuongeza bajeti ya Sekta ya elimu.

Prof. Nombo ametoa shukrani hizo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kutambua mchango wao kwenye Sekta ya elimu

Amesema mchango wa wadau hao umelenga kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu na kwamba hii inaashiria umoja na ushirikiano wa dhati uliopo katika kuboresha Sekta ya elimu