Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda Agosti 29, 2023 jijini Dar es Salaam amefungua Kongamano la Nane la Watafiti wa Kodi Barani Afrika (ATRN) akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Philip Isdor Mpango.
Katika mkutano huo Waziri Mkenda amesisitiza kufanyika tafiti zitakazowezesha kuwa na mifumo bora na yenye tija katika masuala ya kodi ikiwemo kumaliza usafirishaji fedha haramu, wizi wa kimtandao na matumizi ya teknolojia kudhibiti ukwepaji kodi.
Amepongeza hatua hiyo kwamba matokeo ya tafiti zinazofanyika yatawezesha kuwa na Sera za kikodi zinazozingatia hali halisi ya jamii husika.