Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amekabidhi bendera ya Tanzania kwa wanafunzi 30 wanaokwenda nchini China kusoma programu ya uhandisi katika Taasisi ya Chongqing Vocational Institute of Enginnering kupitia Kampuni ya Group Six International & Sino Tan Industrial Park.
Hafla ya kukabidhi bendera hyo imefanyika katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ya jijini Dar es Salaam leo Agosti 28, 2023
Amesema programu hiyo itakuwa ya miaka miwili ambapo wanafunzi wakihitimu watapata diploma ya Taasisi hiyo na miaka hiyo miwili itahesabika kama sehemu ya miaka minne ya Programu yao ambayo wanasoma DIT
“Wanafunzi hawa tayari wameshasoma mwaka mmoja hapa DIT na kufanya mafunzo kwa vitendo kwenye kampuni ya Group Six International & Sino Tan Industrial Park kwa miezi miwili. Hivyo watatumia miaka miwili nchini China na watarejea kumalizia mwaka mmoja hapa DIT na kupata shahada katika eneo hilo,” amesema Waziri Mkenda