
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafadh Ameir amesisitiza kuwa uzalishaji wa wahitimu wenye ujuzi unaolingana na mahitaji ya soko la ajira ndio dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mhe. Wanu amesema hayo mapema leo Februari 9, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa pamoja kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda unaofanywa na Makamu wa Rais Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi.

Amesema jukumu la utoaji wa elimu nchini linahitaji ushirikiano na ndio maana Wizara imezindua Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu ili vijana waweze kutoka vyuoni wakiwa na ujuzi wa kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa taifa.


