
Kongamano la Uandishi Bunifu linaloendelea katika ukumbi wa The Dome Masaki jijini Dar es Salaam litahitimishwa kwa hafla ya Utoaji Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu.

Matukio hayo mawili yamewaleta pamoja wadau wa fasihi na sanaa jioni ya leo Aprili 13, 2026 kusherehekea ubunifu wa Kiswahili, huku mgeni rasmi Abdalatif Abdalla akiheshimisha tukio hili kwa hotuba yake ya kitaaluma na kipekee.

Vipengele vinne vinavyoshindaniwa ni Riwaya, Tamthiliya, Hadithi za Watoto na Ushairi. Hafla hii ni jukwaa la kuenzi mchango wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika kukuza fasihi ya Kiswahili na kutoa nafasi kwa waandishi chipukizi na wakongwe kuonyesha kazi zao bunifu.


