
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejipanga kuimarisha umahiri wa kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto wa elimu ya awali na wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili. Kupitia Mkakati wa Kisayansi, hatua hii inalenga kuweka msingi thabiti wa maarifa na ujuzi wa msingi, ili kuhakikisha kila mtoto anapata nafasi ya kujengewa uwezo wa kitaaluma na kiujuzi mapema.

Wageni mbalimbali wameanza kuwasili katika viwanja vya Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) jijini Dar es Salaam kushuhudia uzinduzi wa mkakati huu muhimu, ambao unatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa elimu ya msingi nchini.

Uzinduzi huu wa Mkakati wa Kisayansi unafanyika Januari 29, 2026, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.


