
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amesema Kampasi ya Lindi itachangia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta ya kilimo kupitia maarifa, Teknolojia, tafiti za kisasa na kutoa suluhisho kwa wakulima.

Mhe. Nchemba amesema hayo Disemba 20, 2025 Mkoani Lindi, baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa Kampasi ya Lindi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Amesisisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kukuza uchumi na kuchochea maendeleo ya Taifa.

Waziri Mkuu ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kusimamia kikamilifu utekelezaji wa Mradi wa HEET kwa ujumla. Aidha ameutaka Uongozi wa UDSM kuanza kutoa mafunzo kwa kasi katika Kampasi hiyo, sambamba na kuzingatia matumizi ya TEHAMA, vifaa vya kisasa vya kufundishia na kujifunzia


