
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, amesema Mradi wa EASTRIP umeleta mageuzi makubwa katika Chuo cha Usafirishaji (NIT) kwa kuanzisha mafunzo ya urubani nchini kwa mara ya kwanza, hatua inayoweka msingi imara wa kuandaa wataalam wa usafiri wa anga ndani ya nchi.

Katika ziara yake NIT Disemba 2025, Mhe. Ameir amesema kuwa Mradi huo umefungua ukurasa mpya katika historia ya mafunzo ya anga, huku Kituo cha Umahiri cha CoEATO kikitoa fursa kwa Watanzania kupata mafunzo ya kimataifa bila kwenda nje ya nchi.

Wanafunzi 22 wamedahiliwa NIT katika fani hiyo, ambapo kundi la kwanza linatarajiwa kuhitimu Machi 2026. Aidha baadhi ya wahitimu wa fani za anga kutoka NIT tayari wamepata ajira nje ya nchi.


