
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, wamewasili na kufanya kikao cha kazi na Wakurugenzi wa Wizara hiyo kama ishara ya kuanza rasmi utekelezaji wa majukumu yao.

Viongozi hao wametumia kikao hicho kujadili utekelezaji wa mipango na vipaumbele vya Wizara, sambamba na kuhimiza kasi na ushirikiano katika kutekeleza mageuzi makubwa ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nchini.


