
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Daniel Mushi, amesisitiza kuwa ujenzi wa kampasi 16 katika mikoa isiyo na Vyuo Vikuu Nchini ni lazima ukamilike kwa wakati ili kufanikisha malengo ya Serikali ya kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya juu kwa vijana.

Amezungumza hayo Novemba 17, 2025 Jijini Dar es Salaam wakati wa Kikao cha pamoja kati ya Wizara na Benki ya Dunia ambapo ameeleza kuwa miundombinu hiyo itakamilishwa kwa wakati ikiwa na Vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili ifikapo mwaka 2026 zianze kutumika kikamilifu.

Kwa upande wake, Benki ya Dunia kupitia ujumbe wake imeahidi kuendelea kushirikiana na Wizara katika kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi. Benki hiyo imesisitiza umuhimu wa usimamizi makini wa rasilimali ili mradi uwe na matokeo chanya kwa taifa, huku ukitarajiwa kuongeza idadi ya wanafunzi wa elimu ya juu, kuimarisha ujuzi wa kisayansi na kiufundi na kuchochea ukuaji wa uchumi.


