Mkoani Morogoro walimu 970 wamepatiwa mafunzo kupitia mradi wa SEQUIP.

Akihitimisha mafunzo hayo Julai 27, Naibu katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia masuala ya elimu Dkt. Hussein Omary akawasisitiza walimu kuhusu matumizi ya TEHAMA ili kuwezesha ambayo kuwafikia wanafunzi wengi hususani wanafunzi katika maeneo yote nchini.



Dkt Hussein amesema matumizi ya TEHAMA yatasaidia kukabilina na changamoto ya upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi

"ukiangalia jiografia ya nchi yetu kuna maeneo baadhi ya masomo huwezi kupata walimu kama tutatumia mfumo huu wa TEHAMA wa Mwalimu mmoja kuwafikia wanafunzi wengi tutafanikiwa" "Amesema dkt Hussein.



Edward Wawa mkurugenzi msaidizi Mafunzo ya ualimu kutoka wizara ya elimu, sayansi na teknolojia amesema dhamira ya serikali ni kuhakikisha walimu wanatumia TEHAMA kama njia ya kuinua ujifunzaji na hatimae matokeo ya wanafunzi .



Amesema katika kutekeleza afua hiyo Mkazo umewekwa katika kuhakikisha walimu wanapata ujuzi wa kisasa unaohitajika katika kufundisha masomo ya sekondari kwa ufanisi zaidi kutumia TEHAMA .

Mmoja wa washiriki wa Mafunzo Jackline Mwakibili, Mwalimu kutoka shule ya sekondari Benjamini mkapa amesema wamenufahika sana na Mafunzo hayo ambayo wanaamini yatawasaidia kuenda na ulimwengu wa kidigitali.