Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26, itaendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria, pamoja na kuandaa miongozo na kutoa mafunzo.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo Mei 12, 2025, Waziri Prof. Adolf Mkenda alieleza kuwa hatua hizi zitaongeza fursa na kuimarisha ubora wa mafunzo ya amali katika shule za sekondari na vyuo vya ufundi, sambamba na kuboresha elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu, na elimu ya juu.



Aidha, Prof. Mkenda alisisitiza kuwa wizara itaendelea kuimarisha uwezo wa nchi katika tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu kwa lengo la kuchangia maendeleo endelevu. Juhudi zaidi zitatumika kuwapeleka vijana wa Kitanzania kusomea masomo ya sayansi ya nyuklia, Sayansi ya Sayansi, na akili bandia katika vyuo bora nje ya nchi