Prof. Ibrahim Noor, Mhadhiri, Mwandishi wa Vitabu na Mchoraji maarufu kutoka Chuo Kikuu cha Sultan Qaboos, Oman, amesema amerudi nyumbani kushuhudia mafanikio ya kazi bunifu za fasihi zinazotekelezwa na Watanzania.



Amewapongeza Watanzania pamoja na familia ya Baba wa Taifa kwa kusherehekea miaka 102 ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwalimu Julius Nyerere ambae alikuwa Mwandishi mahiri katika fasihi.



“ niwapongeze pia Wizara na Taasisi ya Elimu kwa kumuenzi Baba wa Taifa na kuipa Tuzo jina la Mwalimu Nyerere lakini pia kuipa tarehe ya kuzaliwa Kwake kuwa siku maalum ya Tuzo hizi