Mawaziri wa Elimu kutoka mataifa mbalimbali walishiriki mkutano muhimu wa kujadili Mpango wa Rasilimali Watu (Human Capital Initiative) ulioangazia uwekezaji katika watu kama msingi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Prof. Adolf Mkenda, alikuwa miongoni mwa washiriki wa mkutano huo unaofanyika Aprili 13 - 16, 2025 katika Jiji la Riyadh nchini Saudi Arabia. Mjadala ulilenga kuboresha mifumo ya elimu, mafunzo ya kitaaluma, huduma za afya, na sera za ajira ili kuhakikisha watu wanapata stadi, maarifa, na afya bora zinazohitajika kuchangia kikamilifu katika maendeleo

endelevu