Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia inaendelea na  maandalizi ya Mkakati wa kutekekeza ubia (PPP) kati ya sekta ya Umma na Binafsi katika elimu.

Hayo yameelezwa katika kikao kazi cha Menejimenti ya Wizara na Wakuu wa Taasisi na Vyuo Vikuu vya Serikali baada ya kupokea wasilisho juu ya  utekelezaji wa mpango huo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Tanzania ( PPPC) Bwana David Kafulila.

Akizungumza katika kikao kazi hicho Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo amesema ni muhimu kwa Taasisi kuanzisha ushirikiano na wabia katika uwekezaji kupitia PPP ili kuongeza mapato na kuimarisha utoaji huduma.

Kwa upande wake Bw. kafulila ameipongeza Wizara ya Elimu kwa hatua ya kuandaa Mkakati wa ubia katika Sekta, huku akisisitiza juu ya Vyuo Vikuu kuanzisha programu za kuandaa wataalamu wa masuala ya ubia kati ya Sekta Umma na Sekta Binafsi.