Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Januri 13, 2025 amekutana na Balozi wa Tanzania nchini India Mhe. Anisa Kapufi Mbega kwa ajili ya kumshirikisha malengo ya ziara ya kiongozi huyo nchini humo pamoja na kuelekezana masuala kadhaa yanayohusu sekta ya elimu.
Prof. Nombo amemueleza Balozi huyo juu ya Mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini Tanzania.