Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi amekipongeza Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kwa kutekeleza kwa ufanisi ujenzi wa miundombinu mbalimbali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).
Prof. Mushi amefanya zaiara hiyo Januari 10, 2025, ambapo ameshuhudia maendeleo katika kutekeleza ujenzi wa jengo Mtambuka pamoja na madarasa na karakana katika chuo hicho ambayo yamefikia asilimia 75 ya ujenzi.
Aidha amekisisitiza chuo hicho kuendelea kusimamia dira katika kutoa mafunzo ya sayansi na teknolojia, akitilia mkazo mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi wanaosoma fani ya ufundi wa magari ili kuhakikisha Taifa linapata wahitimu mahiri wenye ujuzi unaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
Pia amekitaka Chuo hicho kuendelea kukuza teknolojia ya usindikaji wa maziwa ili huduma hiyo muhimu ipatikane kwa urahisi katika jamii.
Naye Kaimu Makamu Mkuu wa cha MUST, Prof. Zacharia Katambara ameishukuru Serikali kuendelea kuboresha miundombinua ya chuo kupitia Mradi wa (HEET), ambao umewezesha mazingira rafiki ya ujifunzaji