Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Daniel Mushi amesema Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Songwe inaendelea kuimarika kwa haraka katika kuzalisha wataalam sekta ya Ujenzi wanaohitajika katika soko la ajira.
Prif. Mushi ameyasema hayo Januari 09, 2025 Mkoani Songwe katika Mahafali ya Kumi na Nane (18), duru ya tatu, ya Taasisi hiyo kampasi ya Songwe ambapo amesema kuwa Taasisi hiyo inatekeleeza ipasavyo maagizo ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ameongeza kuwa Serikali imeendelea kuongeza fursa za mafunzo na Elimu ya Ufundi na mafunzo ya Ufundi Stadi na kusimamia ubora wa elimu,
"Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali iliongeza udahili katika vyuo vya elimu ya ufundi kutoka wanafunzi 171,581 hadi wanafunzi 235,804" alisema Mushi.
Amebainisha kuwa mafanikio yanayoshuhudiwa katika Kampasi hiyo, yatakuwa yamepatikana kutokana na moyo wa kujituma pamoja na ushirikiano baina ya wanafunzi, wafanyakazi, Menejimenti na Baraza la Taasisi kwa ujumla