Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Januari 08, 2025 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Prof. Haruni Jeremia Mapesa.
Mazungumzo hayo yamefanyika kwa mara kwanza tangu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipomteua Prof. Mapesa kuwa Mkuu wa Chuo hicho Novemba 11, 2024.
Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kipo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia chenye jukumu la kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kuwajengea uwezo viongozi wa umma katika fani ya uongozi na maadili.