Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeibuka Mshindi wa Kwanza katika kundi la Wizara kwenye usimamizi bora wa Rasilimaliwatu.

Tuzo hiyo imetolewa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Mkutano wa Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma uliofanyika Jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Rais Utumishi Vigezo vilivyotumika katika utoaji Tuzo hizo ni uzingatiaji kanuni taratibu na miongozo ya Utumishi, Uzingatiaji Sheria uzingatiaji matumizi ya mifumo ya TEHAMA ikiwemo HR - Assessment, PEPMIS na PIPMIS, e-likizo, utekelezaji bora miundo ya kiutumishi ikiwemo massaging ya Watumishi, usalama na maadili katika utendaji.

Tunashukuru watumishi wote kwa kujituma na kutekeleza majukumu kwa weledi. Tunawatakia utendaji mwema Mwaka 2025 na huduma bora kwa wadau wote.

Asante wateja na Wadau wote wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Heri ya msimu wa sikukuu.