Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia QS Omary Kipanga ameipongeza Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa kuendelea kutoa Elimu Bora na wahitimu mahiri wenye uwezo wa kutatua changamoto mbalimbali za kijamii kupitia Ujuzi wanaoupata wakiwa mafunzoni.



Naibu Waziri amesema hayo, Desemba 13, 2024 akimwakilisha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Faustine Mkenda katika Mahafali ya kumi na nane Duru ya pili katika kampasi ya DIT Mwanza.



Mhe, Kipanga amesema Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, inajivunia maboresho yanaofanyika katika sekta ya elimu ili kuzalisha wataalam wanaoajirika, kujiajiri na kutengeneza ajira kwa wengine.



Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi la DIT, Mhandisi,Dkt. Richard Masika, ameunga mkono hoja ya uboreshaji sekta ya elimu, huku akiishukuru serikali kwa kuanzisha kituo cha ujasiriamali, ubunifu, uhaulishaji wa teknolojia pamoja na malezi ya kampuni kwa Taasisi yake ya DIT